ZANZIBAR ITAENDELEA KUUDUMISHA MUUNGANO-DK.MWINYI

 


Na mwandishi wetu


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar  itaendelea kuwa muumini wa dhati wa Muungano kwa kuudumisha na kuuimarisha kwa faida ya kizazi cha sasa na vijavyo. 


Rais Dk.Mwinyi akizungumza katika kilele cha Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  yalioongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 , Aprili 2024.


Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Imeendelea kupata sifa na heshima kubwa kimataifa kwa kuwa nchi ya mfano kwa kudumu kwa Muungano wa kuwa na amani , umoja na mshikamano .


Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amesema Tanzania  imepata mafanikio makubwa yaliyotokana na Muungano  katika sekta mbalimbali  kiuchumi na huduma za kijamii.


Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewashukuru Viongozi wa awamu zilizopita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada za kudumisha na  kuendeleza malengo ya Tanzania na kuzifanyia kazi changamoto zinazojitokeza na kuzifanyia ufumbuzi.











Post a Comment

0 Comments