Tanzania commercial Bank Baada ya kuzindua huduma ya Toboa na Vikoba Leo pia imeweza kuzindua huduma ya akaunti ya kidigitali ambayo itakayomfanya Mteja alipie bili mbalimbali inayoitwa TCB POPOTE ACCOUNT
Ameyasema hayo Leo Tarehe 30 Julai 2024 Mkurugenzi wa Masoko ukuzaji wa Biashara na mahusiano ya umma Deo Kwiyukwa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam
Amesema Huduma hiyo ya akaunti ya kidigitali unaweza ukalipia bili mbalimbali na ukanunua tiketi ya treni ya Mwendokasi Katika App ya Tcb na Gharama ya kujiunga na TCB POPOTE ACCOUNT ni sh Elfu 1
Nae Afisa mkuu wa huduma za kidigitali na Ubunifu Jesse Jackson Amesema kuwa Tcb ni Bank ya tatu Kwa ukubwa Kwa matawi na inamawakala Elfu Sita Tanzania nzima.
"Tumeiona hiyo haitoshi Bado tunaona kunauwitaji wa kusogeza huduma za kifedha Kwa wateja wetu Kwa nchi nzima takwimu zinaonesha kuwa Asilimia 89 ya watanzania wanaweza kupata huduma za kifedha ndani ya kilomita 5 na pia Asilimia 22 tu ya watanzania ambao wanaakaunti za kibank, na Bado kunauwitaji wa kusogeza huduma hizi za kifedha pia kurahisisha huduma za kifedha Kwa gharama nafuu sana". Amesema Jackson
Aidha Amesema kama Tcb ni Bank ambayo inayomuelewa mtanzania Zaidi na imeleta huduma ya TCB POPOTE ACCOUNT ambayo mtanzania au Mteja Wowote anaweza kuifungua Mahali popote alipo Kwa simu yake ya mkononi na anachoitaji ni namba yake ya nida au kitambulisho na anaweza kufungua akantu Kwa kutumia maelekezo ya ndani ya dakika 2
Jackson Ameongeza kuwa wamewuwezesha Mteja kutumia huduma hiyo Kwa huduma mbalimbali Kulipia bili,Mikopo,na kukata tiketi za SGR kwa kulipia Kwa mawakala Zaidi ya elfu 600 ambao wanapatikana Tanzania nzima
0 Comments