SERIKALI YAAHIDI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI KATI YA WANANCHI NA JESHI LA MAGEREZA WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA

 




Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imepokea malalamiko ya mgogoro wa Ardhi kati ya Wananchi na Jeshi la Magereza katika Kijiji cha Rusumo Wilayani Ngara Mkoani Kagera.


Kauli hiyo imetolewa Julai 30, 2024 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo wakati akizungumza na Wananchi wa kata ya Rusumo Wilayani Ngara Mkoani Kagera baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kutazama mgogoro uliopo baina ya Wananchi na Jeshi la Magereza.


Mhe. Sillo amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, nisikivu hivyo suala hilo la mgogoro huo atalifikisha katika vikao vya kamati ya maamuzi ili liweze kutatuliwa.


“Niwaombe wakazi wa kata na Kijiji hiki cha Rusumo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapenda sana na sisi kama Wizara tumewekwa kwa ajili ya kumuwakilisha yeye ili kutatua changamoto zenu, suala hili la Mgogoro huu nimelichukua na tutalishughulikia”

Post a Comment

0 Comments