CDE: BANANGA AWAFUNDA VIJANA WA CCM KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

 




Na mwandishi wetu


Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ally Bananga amewataka Vijana wa CCM Wilaya ya Kinondoni kuwa wamoja na kuwa na kauli Moja ya Ushindi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024. 


Ndugu Bananga ameyasema hayo alipokua anazungumza na Wajumbe wa Baraza la UVCCM Wilaya ya Kinondoni tarehe 22 Agosti, 2024 ambapo alikua Mgeni Rasmi kwenye Baraza hilo.


"Vijana mnapaswa kudumisha umoja miongoni mwenu kuhakikisha kuwa mnakua wamoja na kauli moja kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na mjue kabisa takwa la kikatiba la CCM ni kushinda uchaguzi na kuongoza Dola" 


"Ninyi ndio askari wa Chama hiki, mnapaswa kujua nafasi zenu katika kukihakikishia Chama Ushindi wa kutosha, lakini pia ninyi wenyewe msiwe wabeba watu tu, Wakati ukifika na ukajipima  nenda kavute fomu ugombee nafasi hizo ni za kwenu pia" alisema Cde Bananga.


#TunaendeleaNaMama

Post a Comment

0 Comments