📍 NYAMAGANA - MWANZA
🗓 12 Agosti 2024
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), *Ndg. Suzan Peter Kunambi (MNEC)*, amesema amefurahi kuona fedha zilizotumika zinaendana na shule hii nzuri na yenye viwango, ambapo zaidi ya Tsh milioni 584 zimetumika.
Amesema hayo leo tarehe 12 Agosti 2024 alipotembelea na kukagua Mradi wa Shule ya Sekondari Stanslaus Mabula ilipo Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza ,Lengo la UWT ni kuhakikisha utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 unafanyika kwa vitendo.
Aidha, ameongeza kuwa lengo la Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa, ni kuleta miundombinu mbalimbali ya maendeleo katika kila Vijiji na Vitongoji.
Kunambi amesema amefurahi kuona wanafunzi watapata elimu katika mazingira mazuri, ili wapate elimu bora kwa ajili ya kujikimu katika maisha yao. Mradi huu pia umepunguza masafa ya kutembea kwa wanafunzi.
Ametoa wito kwa wanafunzi wasome kwa bidii, wawe na heshima kwa walimu na wenzao, na wamtangulize Mungu katika kila jambo ili wafanikiwe.
Pia, amewataka walimu na wanafunzi kuutunza mradi huu ili udumu kwa muda mrefu na wanufaike wao na wengine Watakao kuja
#uwtimara
#jeshiladktsamiadktmwinyi
#ushindinilazima
#mitanotena
0 Comments