MWENYEKITI WAZAZI TAIFA AWATAKA WAKANDARASI KUMALIZA MIRADI KWA WAKATI

 




Na mwandishi wetu


Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Ndugu Fadhili Rajab Maganya (MCC) amekagua ujenzi wa Daraja Kata ya Makuyuni Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro lenye thamani ya Shilingi Milioni Mia Nne Ishirini na Tatu (423,000,000)


Ambapo amewaasa Wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha Mradi huo ukitekelezwa, 


Aidha Ndg. Maganya amewaasa wakandarasi kutekelelza miradi kwa wakati kwani wananchi wanakuwa na shauku ya Kutumia miradi hiyo na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika miradi hiyo. 


Pia Ndg. Maganya amekagua Shule za Jumuiya ya wazazi na Shule za serikali ambapo ametoa maelekezo mbalimbali katika Miradi hiyo ya Chama na Serikali. 


Ndg. Maganya yuko Mkoa wa Kilimanjaro kwa Ziara ya Siku tatu ambapo ya kuimarisha Chama na Jumuiya zake.








Post a Comment

0 Comments