Na mwandishi wetu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema miongoni mwa mafanikio makubwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayojivunia ni ushirikiano wa Kidiplomasia uliopo baina yake na Serikali ya India kwa kuanzishwa tawi la Chuo Kikuu cha Teknolojia cha IIT Madras, Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Balozi wa India nchini, Mhe. Bishwadip Dey aliyefika kujitambulisha Leo tarehe: 20 Agosti 2024, Ikulu Zanzibar
Amesema, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha IIT Madras ni fursa muhimu kwa sekta ya elimu Zanzibar itakayoleta mageuzi makubwa ya mifumo na kukuza teknolojia nchini.
Rais Dk. Mwinyi ameiomba India kupitia mtandao mkubwa wa teknolojia walionao na kwa uweledi wa mitandao ya kijamii kuendelea kuitangaza Zanzibar Kimataifa kupitia tawi la Chuo hicho duniani pamoja na sekta za biashara na uwekezaji.
Naye, Balozi Bishwadip Dey alimuhakikishia Rais Dk. Mwinyi kuendeleza historia ya ushirikiano uliopo wa pande mbili hizo hasa kwenye kuboresha sekta za Biashara, Uchumi, Utalii na Uwekezaji pia alimuahidi Rais Dk. Mwinyi kuendelea kupokea wafanyabiashara wakubwa kutoka India, wenye nia ya kuwekeza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
@ikulu_habari
@dr.hmwinyi
0 Comments