RC CHALAMILA AFANYA ZIARA YA KIMKAKATI JIMBO LA KIBAMBA WILAYA YA UBUNGO.

 





Na mwandishi wetu


-Akagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kufanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa mpira Makuti Kata ya Msigani.


-Amshukuru Rais Dkt Samia kwa kutekeleza miradi Lukuki katika Wilaya hiyo. 


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila leo Agosti 13,2024 amefanya ziara ya kukagua miradi  mbalimbali ya maendeleo, kisha kufanya Mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwapatia Wananchi fursa ya kutoa kero zao na kuzipatia majawabu papo hapo.


RC Chalamila akiwa katika Jimbo la kibamba wilaya ya Ubungo amekagua ujenzi wa mradi wa nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ambapo ametoa maelekezo kwa mkandarasi wa ujenzi huo kukamilisha ujenzi haraka ili mradi huo uanze kutumika mara moja, 


Vilevile RC Chalamila alitembelea barabara ya Matosa - Temboni yenye urefu wa kilomita 3 pamoja na mradi wa maji(DAWASA) katika kata ya Kwembe.


Aidha Mhe. Chalamila amepongeza Wilaya ya Ubungo hususani Jimbo la Kibamba kwa jitihada wanazofanya katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa nyingi ambazo zimefanikisha utekelezaji wa miradi mingi katika Jimbo hilo tena miradi yenye masilahi mapana kwa wananchi. 


Sanjari na hilo RC Chalamila ameonesha kutokuridhishwa na mradi wa maji katika kata ya Kwembe na kuwataka mamlaka husika kuweka mikakati inayoeleweka ya kutatua kero za wananchi walioonekana kulalamikia ukosefu wa maji katika maeneo hayo hivyo ameagiza tatizo hilo lishughulikiwe ndani ya muda mfupi.


Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Hassan Bomboko amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kufanya ziara ambapo amemhakikishia kutekeleza maagizo na maelekezo yake mapema iwezekanavyo ili kuleta ustawi wa wana kibamba.







Post a Comment

0 Comments