DOYO AMEWATAKA WANASIASA NCHINI KUFANYA SIASA ZA KISTAARABU

 


Na mwandishi wetu

KATIBU Mkuu wa Chama Cha National League For Democracy(NLD) Doyo Hassan Doyo  amewataka wanasiasa nchini kufanya siasa za kistaarabu na kuacha kutumia lugha zisizo na staha.

Doyo ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam jana wakati wa uzinduzi wa operesheni ya fyeka Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyoenda sambamba na kuwapokea wanachama mbalimbali.

Alisema siasa  zinazofanywa na wanasiasa zisisababishe maisha mengine kuharibika na kutengeneza uhasama na kupelekea watu kununiana pamoja na  kusalimiana .

" Siasa lazima zifanyike katika mazingira yanayoheshimika ..wanasiasa tuheshimiane .. wanasiasa tusifanye kiburi kwa viongozi ambao wako madarakani," Nakuongeza kuwa" kwa uelewa wangu siasa ni tunu inayosogeza  maendeleo kwa wananchi "alisisitiza Doyo 

Aliongeza kuwa viongozi  nchini wanapaswa kutokufanya siasa ambazo zitakwenda kuzalilisha watu .

"Juzi tunasikia kuna kongamano lilifanyika nchini la wanawake wanaosadikiwa kuwa ni Wanachama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanasema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni muuaji maneno haya katika siasa sio mazuri tena yenye tafsiri mbaya  kwenda kumtuhumu Kiongozi wa nchi ni muuaji ni kuikosea siasa za Tanzania na wananchi awawezi kuendeshwa kwa siasa za namna hiyo hivyo ni muhimu kuwa wastaarabu"alisema Doyo

Aidha alisema Chama cha NLD kinaamimi katika itikadi ya uhuru ambao una mipaka na usio na shida ya kutukana watu ili upate watu.

"Chama Cha NLD kinakuja kuonesha njia ni Chama mbadala kinachokwenda kushika dola kwani tunasera na itikadi nzuri NLD inaamini katika haki na uzalendo "alisema Doyo

Aidha  ameiomba Ofisi ya Rais tawaka za Mikoa na Serikali za mtaa(TAMISEMI)kusogeza mbele Uchaguzi wa Serikali za offza mtaa kwani muda wa kujiandaa uliowekwa ni mdogo.

"Tunaiomba TAMISEMI irekebishe ratiba ya Uchaguzi wa Serikali siku za mchakato ziongezwe ili vyama vya siasa viweze kujipanga vizuri"alisema

Akizungumzia kuhusu Programu waliyoizindua Doyo alisema itakwenda kutembelea mikoa 10 ambayo ni pamoja na Tanga, Lindi, Mtwara, Ruvuma,Mbeya, Singida, Dodoma,Mwanza na Kagera.

Alisema kupitia programu hiyo watategeneza  wagombea ambao wataweza kushindana kwa hoja.






Post a Comment

0 Comments