ENNOVATE VENTURES YAFUNGUA MILANGO KWA WAJASILIAMALI WA AFRIKA

 


Na mwandishi wetu

Ufadhili unaotolewa na Taasisi ya ennovate ventures inayojihusisha na Katika kukuza Uchumi wa Afrika kwa kuwashika Mkono Katika biashara zinazoanza na Kukua ambayo wajasirimali wataongezewa usaidizi wa mtaji,Masoko na Mbinu Katika biashara.


Akizungumza Leo Jumatano Septemba 26,2024 na waandishi Habari Jijini Dar es salaam Mkuu wa Masoko kutoka Ennovate Ventures Jasmin Abdallah amesema wanatoa ushauri wa kibiashara kwa wajasiliamali wanaoanza biashara kwa lengo la kukuza biashara zao kwa sababu wamegundua wajasiliamali Wengi wana changamoto hawapati Taarifa sahihi za fursa Mbalimbali.


"Tunaona sasa hivi wawekezaji wengi Duniani wanakuja kuwekeza Afrika na macho yao wameelekeza pia Tanzania,lakini tumegundua wajasiliamali wengi wana changamoto na hawapati Taarifa sahihi za Uwepo wa fursa zilizopo"


"Cha kwanza tunachofanya ni tathimini kuelewa Kampuni yako iko Katika hatua gani ,shida inayokukabili na msaada unaohitaji kupeleka bidhaa zako nje au huwezi kupata 'Board members' ,tunatoa pia ufadhili kuanzia dola 10,000 mpaka dola 20,000"amesema Jasmine Abdallah

Post a Comment

0 Comments