MIL.28.8 ZA REGROW ZANUFAISHA KIKUNDI CHA COCOBA MIKUMI



 


Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) umenufaisha kikundi wa  kijamii cha COCOBA Chekereni Mikumi Mkoani Morogoro kwa kutoa shilingi milioni 28.8  huku wakimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujali vikundi vya kijamii ili kujikwamua kiuchumi. 


Akizungumza katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii , Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) amefurahishwa na maendeleo ya kikundi hicho kinachojishughulisha na uchakataji wa mafuta ya kupikia huku akiwataka kuendelea kujiimarisha zaidi. 


Katika hatua nyingine, Mhe.Mnzava  amewahimiza wanakikundi hao kujishughulisha na shughuli za uhifadhi huku akiwataka wawe mstari mbele kupinga   vitendo vya ujangili wa Wanyamapori.



Naye, Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb)amewataka kutumia fedha walizopewa na Serikali kwa manufaa yaliyokusudiwa ili kukuza vipato na uchumi wao.


Awali, akiwasilisha taarifa ya kikundi, Mwenyekiti wa kikundi cha COCOBA Chekereni, Rehema Njovu amesema kupitia Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW ) wamepokea takribani shilingi milioni 28.8.


Amefafanua kuwa kupitia fedha hizo wamefanikiwa kupata mikopo yenye riba nafuu, kumudu gharama za maisha, kusomesha watoto na kupata faida itokanayo na mashine ya kuchakata mafuta ya kupikia.


Ziara hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi na Watendaji na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Hifadhi ya Taifa Mikumi.






Post a Comment

0 Comments