SHULE ZA SAFI KINARA KATIKA KUINUA VIPAJI

 




Na mwandishi wetu

SHULE za awali na Msingi za Safi zilizopo Jijini Dar es salaam zinag'ara katika kuinua na kuendeleza vipaji mbalimbali kwa vijana ,katika ngazi na rika tofauti ikiwa ni pamoja na kuboresha afya na kujenga mshikamano

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika fainali za michezo ya mpira wa miguu ,Meneja wa shule za Safi ,Ndg Paul Assey amesema Kuwa imekua sehemu ya tamaduni na utaratibu wao kuanzisha mashindano mbalimbali kila ifikapo mahafali ya shule zao kila mwaka ikiwa ni sehemu yakunoa vipaji

'Kila mwaka tunapoelekea mahafali yetu ni lazima tuanzishe haya mashindano ikiwa ni sehemu yakuinua vipaji na kuendeleza" Alisema Paul Assey

Katika fainali za leo mshindi wa kwanza alijitwalia Kombe ,huku mshindi wa pili akipata jezi na wa tatu mpira na zawadi nyingine kemkem.




































Post a Comment

0 Comments