TAMWA YAZINDUA MAKALA MAALUM KWA ELIMU BORA NA ELIMU JUMUISHI

 







Na mwandishi wetu

Chama Cha Wanahabari wanawake Tanzania TAMWA imezindua Makala yake mpya inayoangazia elimu Bora na Elimu jumuishi Kwa wanafunzi Katika shule za umma

Makala hiyo ni Kampeni ya kipindi Cha mwezi mzima  inayolenga kuelimisha jamii Kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto shule Kwa wakati,hasa wale waliohatarini zaidi.kuacha shule na inalenga kuwafikia walimu Zaidi ya 200

Ameyasema hayo Leo Tarehe 23 September 2024, Meneja Mradi TAMWA Servia Daulinge Amesema Makala hiyo inatoa uchambuzi wa kina Kuhusu changamoto zinazowakumba makundi yaliyotengwa kama vile wasichana, watoto wenye ulemavu,na watoto kutoka familia maskini,huku ikipendekeza suluhisho la kuhakikisha watoto wote wanapata elimu Bora.

“Makala imeleta pamoja sauti za watoto,Wazazi,Walimu,mashirika ya kiraia (CSOs),na Afisa wa serikali,ikianzisha mazungumzo Kuhusu jinsi ya kuvunja vikwanzo vinavyowazuia watoto kupata elimu Bora na sio Bora elimu,pia inasisitiza haja ya haraka ya kukabiliana na changamoto hizi Kupitia uwezeshaji wa jamii, ushirikiano na watu wenye ushawishi,na kuboresha sera za elimu Nchini”.Amesema Daulinge

Aidha Daulinge anasisitiza haja ya sera na mikakati.inayolenga kusaidia makundi hatarishi kama vile wasichana, watoto wenye ulemavu, watoto kutoka familia maskini na watoto kutoka jamii zilizo pembezoni Kwa kuboresha mazingira ya shule wanaweza kufanikisha.elimu Bora na watoto kufurahia kwenda shule.

Daulinge ameeleza kuwa ushirikiano wa pamoja utasaidia kuhakikisha uwakilishi mzuri wa changamoto za kipekee zinazowakumba watoto Katika mazingira mbalimbali,na utofauti huo unatoa taswira ya kina na Pana ya hali ya elimu Nchini ambayo itasaidia kubadilika Kwa mazingira ya ufundishaji na uandikishwaji wa watoto Kwa wakati Ili kupata kizazi kinachopenda elimu.

“Kila mtoto anastahili elimu bora,elimu jumuishi na yenye usawa,sio tu Kuhusu mustakabali wao,Bali ni mustakabali wa jamii yetu nzima,kuvunja vikwazo,tunaweza kuunda fursa Kwa watoto wote kustawi,Tushirikiane na kufanya elimu kuwa kipaumbele Kwa kila mtoto pamoja tunaweza Kujenga kesho iliyo Bora”.

“Watoto wanaacha shule hasa Katika maeneo yenye uhaba wa huduma hii inatokana na umaskini,umbali mrefu wa shule,Mila na desturi za kijamii zetu na ukosefu wa rasilimali za kutosha za muweza mtoto kwenda shule, watoto wenye ulemavu wanakubwa Zaidi na hali hii Kwa sababu nyingi ya shule hazina miundombinu au rasilimali za kukidhi mahitaji Yao ya kielimu”,Ameelezea Daulinge

Hata hivyo Daulinge amewasisitiza wazazi na walimu kuwa uwazi Kuhusu kuhakikisha watoto wanapata elimu Bora na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kufanya shule ziwe jumuishi na usawa,kama watetezi wa mstari wa mbele wa haki za watoto,wameona ni muhimu na ni majukumu Yao Katika kukuza elimu jumuishi na kuhakikisha kila mtoto anapata elimu Bora.

TAMWA,Kwa kushirikiana na shirika la kimataifa lisilo la kiserikali-WE WORLD Chini ya “EDUCATION ABOVE ALL” ambalo limesaidia mradi wa PAMOJA TUDUMISHE ELIMU Inaendelea kushirikiana na wadau wengine kitekeleza haki ya elimu Kwa wote

Post a Comment

0 Comments