UKAGUZI WA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM (2020-2025) WILAYA YA KINONDONI.

 







📍 CCM (W) Kinondoni 

🗒️ 05 Septemba, 2024


Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kimekua na utaratibu wa kikatiba wa kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kila baada ya miezi 6. 


Katika kipindi cha miaka minne (2020 hadi 2024) Katika Wilaya ya Kinondoni Serikali imeendelea kuimarisha maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na kisiasa kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Aidha kazi hizi ni sehemu ya ahadi za CCM kwa wananchi, zinazotekelezwa kwa nia ya kuboresha maisha ya Wananchi wa Kinondoni.


Ukaguzi huu ulilenga kupima kiwango cha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya ya Kinondoni. Pia, ni fursa ya kuangalia changamoto zilizopo na kuweka mikakati mahsusi ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa ahadi kwa kipindi kilichosalia.


CCM Wilaya ya Kinondoni inajivunia na kumpongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyotoa fedha nyingi za Maendeleo Wilaya ya Kinondoni,  mafanikio makubwa yaliyopatikana ni matokeo ya mchango wake mkubwa, lakini tunaendelea kujipanga kuhakikisha tunatimiza ahadi zote kabla ya mwaka 2025.


Miradi iliyotembelewa ni,  


Kikundi Cha kina Mama ambao ni wanufaika wa Mikopo ya Halmashauri cha (Weaving Point) Kata ya Bunju kinachojuhusisha na useketaji wa masweta kilichokopeshwa Million 38.2, 


Ujazaji wa Kifusi kuondoa maji yaliyotuqna shule ya Msingi Michael Urio Kata ya Kunduchi wenye thamani ya shilingi milioni 147, 


Ujenzi wa Barabara ya Kawe Sokoni Kata ya Kawe yenye thamani ya shilingi Milioni 755.9, 


Kikundi cha Vijana wanaojihusha na Usafirishaji wa abiria cha (Chamabavi) waliokopeshwa shilingi milioni 125, 


Upangaji wa Wafanyabishara katika Soko la Tandale kata ya Tandale lililogharimu Bilioni 10.47


Aidha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Ndugu Shaweji Mkumbula, ametoa maelekezo kwa viongozi wa wilaya kuhakikisha kuwa wanufaika wote wa mikopo ambao wanaendelea kurejesha mikopo yao kwa ufanisi waaangaliwe  kwa lengo la kuwaongezea mtaji au kuwapa Msaada ili kuwawezesha kukuza biashara za.


Pia, ameagiza viongozi hao wasaidie wanufaika hao kupata masoko ya uhakika kwa bidhaa au huduma zao ili kuhakikisha wanapata faida endelevu, jambo litakalosaidia kuongeza tija kwa mikopo wanayopewa na kuzialisha ajira nyingi zaidi kwa Vijana ambazo zitasaidia kuwaimarisha kiuchumi.


Mwisho, Mwenyekiti amewasihi Viongozi wa Wilaya kuboresha Changamoto ndogo ndogo zilizoainishwa na wafanyabishara wa soko la Tandale Ili kuwawezesha wafanyabishara hao kufanya kazi zao katika mazingira rafiki kwa kuwahakikishia usalama wa bidhaa zao.








Post a Comment

0 Comments