UWEKEZAJI WA TRILIONI 6.55 MRADI WA JNHPP WALETA TIJA NCHINI.

 





Na mwandishi wetu

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC) Leo tarehe 11 Septemba, 2024 imetembelea ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere JNHPP na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi ambao kwa sasa umefikia asilimia 98.99


Akizungumza kwenye ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa kamati  Mhe.Marry Masanja(MB) amesema kuwa Uwekezaji uliofanywa na Serikali kwenye mradi huo ni wenye Tija kwani umeleta ongezeko la umeme wa kutosha kwenye Gridi ya Taifa na kutoa fursa kwa Watanzania kupata ajira mbalimbali katika mradi  wakati wa utekelezaji wa ujenzi wa mradi.


"Serikali imewekeza kiasi cha  Shilingi Trilioni 6.55,fedha za watanzania ,ili kuweza kujenga mradi huu,mpaka sasa kiasi cha Trilioni  6.15 tayari zimeshalipwa kwa mkandarasi ,na mara mradi huu utakapokamilika tutaweza kuwa na umeme mwingi zaidi na hivyo tutaweza kuuza Umeme  katika nchi za jirani" alisema Mhe. Masanja


Aliongeza  kwa kusema  kuwa kama kamati inayosimamia masuala ya wekezaji wa Serikali imeridhishwa na Uwekezaji uliofanywa katika ujenzi wa mradi wa JNHPP na kuitaka Serikali kuendelea kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya kimkakati


"Nimpongeze Raisi wetu Mama Samiah Suluhu Hasan, ameweza kusimamia mradi huu mkubwa wa kimkakati na kutenga fedha kwajili ya  ujenzi wa Mradi huu  ambao ivi leo umefikia asilimia 98.99,ni mradi wa kujivunia kwa kila mtanzania,na niombe Serikali kuendelea kuwekeza kwenye miradi ye ye tija kama hii" alisema  Mhe.Masanja


Naye Mmoja wa mjumbe wa kamati hiyo,Mhe.  Nicholaus  Ngassa,

ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Igunga-Tabora amesema kuwa kupitia mradi wa JNHPP hali ya Umeme imeimarika  nchini, na  katika jimbo la Igunga wananchi wengi tayari wanahuduma ya Umeme,


"Hali ya Umeme inaendelea kuimarika,Igunga wananchi wengi wana Umeme,nitoe rai kwa wananchi wa Igunga na maeneo mengine,tuutumie umeme huu kwa faida yetu, hasa katika kutunza mazingira kwa kuanza kutumia umeme kama nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa,umeme upo na gharama ni nafuu" alisema Mhe.Ngassa 


Aidha,Naibu Katibu Mkuu wizara ya Nishati Mha.James Matarajio amesema kuwa mpaka sasa mitambo 3 imeshaanza kufanyakazi katika Mradi huo,ikiwa ni mashine namba 9,8 na namba 7ambazo zimeshaongeza umeme wa megawati 705  kwenye Gridi ya Taifa ,na mashine nyingine mbili tayari zipo kwenye majaribio  ambapo mashine namba 5 itawashwa mwezi Novemba na mashine nyingine namba 3 itawashwa mwanzoni mwa mwaka 2025 na kuleta jumla ya megawati 2115.


Sambamba na hilo Mhe.Mataragio ameishukuru kamati hiyo kwa kutembelea mradi.






Post a Comment

0 Comments