KAMATI TENDAJI YA MRADI WA SOFF YAKUTANA KUIDHINISHA MPANGO KAZI WA UTEKELEZAJI WA MRADI TANZANIA

 

KAMATI Tendaji ya Utekelezaji wa Mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuimarisha Uangazi wa Hali ya Hewa (SOFF), imekutana kwa mara kwanza katika ukumbi wa hoteli ya Morena, Morogoro, Ikiwa na lengo la kupitia na kuidhinisha Nyaraka muhimu za kuanza rasmi utekelezaji wa mradi huo nchini Tanzania.

Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dk. Ladislaus Chang'a aliwashukuru wajumbe wa kamati tendaji kwa kukubali kuwa sehemu ya kusimamia utekelezaji wa Mradi wa SOFF Tanzania. 

 Dk. Chang’a alitoa shukrani zake za dhati kwa Sekretarieti ya SOFF na WMO, kwa kuichagua Tanzania kuwa miongoni mwa wanufaika wa ufadhili wa fedha za Mfuko huo takribani dola za kimarekani milioni 9.

"Uwepo wenu ni ushahidi tosha wa dhamira yenu ya kusaidia kuboresha huduma za hali ya hewa kwa nchi yetu, kikanda na Duniani kote, huduma ambazo zitaenda kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi”, alisema Dkt. Chang'a.

Dk. Chang'a aliongeza kuwa uanzishwaji wa mradi wa SOFF utasidia nchi kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa data za hali ya hewa na mfumo wa mawasiliano wa ubadilishanaji wa data hizo kimataifa kwa kuwezesha masuala ya muhimu ya kiufundi na kifedha.





Post a Comment

0 Comments