MIKATABA YA UJENZI WA KM 168 ZA BARABARA YASAINIWA

 





DAR ES SALAAM


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Oktoba 24, 2024 ameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya awali ya ujenzi wa zaidi ya kilomita 168 za barabara za Mkoa wa Dar es Salaam, zitakazojengwa na mradi wa DMDP awamu ya pili.

Akizungumza katika hafla hiyo mkoani Dar es Salaam, Mchengerwa amesema jumla ya zabuni 19 tayari zimetangazwa na zipo katika hatua mbalimbali za manunuzi ambapo kati ya zabuni hizo leo umefanyika utiaji saini wa mikataba nane ya awali yenye thamani ya shilingi Bilioni 190.04 inayokwemda kujenga jumla ya kilomita 63.66 za barabara.

Mchengerwa amesema kwa mikataba iliyobaki yenye thamani ya shilingi Bilioni 262.46, zitajengwa kilomita 104.56 za barabara ambapo ndani ya mwezi Novemba 2024 itakuwa imekwishasainiwa.

Mradi wa DMDP awamu ya pili unatarajiwa kuboresha miundombinu mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam zikiwemo barabara, masoko, vituo vya mabasi, mifereji ya maji ya mvua, maeneo ya wazi pamoja na usimamizi wa taka ngumu.






Post a Comment

0 Comments