Mkuu wa Mkoa wa Arusha,amzawadia gari jipya,la kisasa na lenye thamani kubwa Sheikh wa Mkoa huo

 





*_Mkuu wa Mkoa wa Arusha,amzawadia gari jipya,la kisasa na lenye thamani kubwa Sheikh wa Mkoa huo_*.


*_Tusipowathamini sisi kutokana na kazi kubwa wanazozifanya,Allah Mtukufu atawaweka kwenye nusura zake_*.


Na Hamimu H.Mussa,Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Paul Makonda,amemzawadia zawadi ya gari la kisasa aina ya Range Lover-Discovery,huku akisema kuwa kama Mkuu wa Mkoa huo,amekuwa akifanya kazi vizuri na Viongozi wa Kidini huku akimwezea Sheikh ShabaniJuma,kama Sheikh wa Mkoa huo mwenye mchangango mkubwa katika kuuendeleza Mkoa wa Arusha.

Mheshimiwa Makonda,amesema kuwa ametoa zawadi hiyo ili Kiongozi huyo aendelee kutimiza kiurahisi majukumu yake ya kumtumikia Mwenyeezi Mungu,na Waislaamu kwa ujumla.

Akiongea baada ya kupokea zawadi hiyo katika mshuko wa Swala ya Ijumaa jana tarehe 25/10/2024,na akiwa mbele ya mamia ya waumini wa dini ya Kiislaamu pamoja na wakazi wa Mkoa huo,Sheikh Shabani Juma(Sheikh wa Mkoa),amemshukru ndugu Makonda na mwakilishi wa Mheshimiwa Rais,kwa kuamua kutoa zawadi hiyo kwake na kwa Waislaamu wa Arusha.

Amesema kuwa,kwake ni jambo kubwa limefanywa na Mheshimiwa Makonda kwani,hakulitegemea huku akiwasisitiza watu kuendelea kumtumikia Allah Mtukufu tena kwa wema,uadilifu,uaminifu,kujitoa na kujituma wakitaraji malipo makubwa kutoka kwa Allah Mtukufu.

Zaidi ya hapo,Sheikh Shabani ametumia fursa hiyo,kumshukru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani,kwa kuwapelekea Mkuu wa Mkoa huo mpenda watu na asiye na ubaguzi,mweledi,mcheshi na anayetekeleza majukumu yake ya Kiserikali kwa kuwashirikisha wengine.

------------------Mwisho------------------

Post a Comment

0 Comments