Na mwandishi wetu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amemaliza ziara yake ya siku mbili nchini Qatar.
Rais Mwinyi na ujumbe wake ameagwa na viongozi waandamizi wa Qatar katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hamad International Airport uliopo Doha wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini humo Balozi Habibu Awesi Mohamed.
Katika ziara yake hio Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi alishiriki Mkutano wa Kimataifa wa kutimia miaka Thelathini ya Familia Duniani, Kutembelea Taasisi ya Qatar Charity na Qatar Foundation na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na viongozi wa juu wa nchini humo akiwemo Waziri anaeshughulikia masuala ya Wakfu Mhe.Shanem bin Shaheem bin Ghaneem Al-Ghanim
Akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,Rais Dk.Mwinyi amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Chama Cha Mapinduzi, Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya SMZ na SMT, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa.
0 Comments