WANU H. AMEIR - KUPATA ELIMU YA AFYA NI JAMBO MOJA, LAKINI MUHIMU SANA NI KUPIMA KUJUA AFYA YAKO

 


*WANU H. AMEIR - KUPATA ELIMU YA AFYA NI JAMBO MOJA, LAKINI MUHIMU SANA NI KUPIMA KUJUA AFYA YAKO*

"Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) tunaunga mkono Serikali zote mbili, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika masuala ya Elimu, Afya na Uchumi" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF)

"Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) katika Elimu, MIF imeweza kukuza ufaulu na kupunguza Sifuri katika Mkoa wa Kusini Unguja kwa Asilimia 84. Mwaka 2022/2023 kutoka Asilimia 68 kwa Mwaka 2020/2021" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), Mwenyekiti MIF 

"Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) tumeweza kuwasomesha Wanafunzi walioshindwa kuendelea na Elimu ya Juu mafunzo ya Amani takribani Wanafunzi 114 katika Vyuo vya Amani ikiwemo Makunduchi na Mkokotoni" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), Mwenyekiti MIF 

"Katika suala la Afya, Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) tumekuwa tukishajihisha Vijana, Wanawake na Wanaume kwenye Afya ya Akili kupitia Semina mbalimbali na Michezo kama vile Marathon, Netball, Football na Michezo mingine mbalimbali" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), Mwenyekiti MIF 

"MIF kwenye masuala ya Afya, tumeweza kuwabadilisha akina Mama takribani 2,000 kutoka kwenye matumizi ya Nishati Chafu (Kuni na Mkaa) na kuwapeleka katika matumizi ya Nishati safi na salama ya kupikia kwa kuwapatia mitungi ya gesi. Hii ni kuunga mkono jitihada za Serikali zetu mbili" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), Mwenyekiti MIF 

"Lengo la MIF kubeba Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia ni kuwakinga akina Mama kutokana na madhara ya kutumia Kuni na Mkaa ambapo hupata athari kutokana na moshi wakati wa kupika" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), Mwenyekiti MIF 

"Katika kuadhimisha Siku ya Saratani Duniani, Taasisi ya MIF ikishirikiana na Taasisi ya Huduma ya Afya Aga Khan na Wizara ya Afya Zanzibar tumeandaa siku mbili Maalum ya maadhimisho kwa kuipa kipaumbele jamii kupata elimu juu ya Saratani ya Matiti na Saratani ya Nyonga ya Kizazi na Tezi Dume kwa upande wa akina Baba na kufanya uchunguzi wa awali wa Saratani hizi" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), Mwenyekiti MIF 

"Nichukue nafasi hii niwaombe wale wote waliofika hapa wasikose kupima Saratani hizi kwasababu hivi sasa imeshakuwa nyingi miongoni mwetu na hamna namna, inabidi na ni lazima tupime, nawaomba sana hasa akina Mama" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), Mwenyekiti MIF 

"Tafiti zinaonyesha ugunduzi wa awali wa Saratani huokoa maisha  kwa asilimia kubwa sana, hivyo nipende kuwasisitiza wananchi wenzangu kuweza kujijengea utamaduni wa kujichunguza mara kwa mara na pindi utakapoona au kuhisi viashiria waende kituo cha Afya kwa uchunguzi zaidi" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), Mwenyekiti MIF 

"Kupata elimu ni jambo moja lakini jambo la muhimu sana ni kupima ili kujua Afya yako. Nasisitiza tena hasa akina Mama kwasababu mara nyingi sana ndiyo waathirika wakubwa wa maradhi ya Saratani" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), Mwenyekiti MIF 

"Inawezekana umeanza Kupata dalili za mapema za Saratani lakini hujui kuwa ndiyo dalili zenyewe. Moja ya dalili kwa akina Mama tukiwa kwenye siku zetu tunatokwa na damu sana. Tuna mtindo wa kusema mke mwenza kaniroga, Hapana!" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), Mwenyekiti MIF

Mwisho, Mhe. Wanu Hafidh Ameir ametoa Shukrani za dhati kwa Wizara ya Afya Zanzibar, Waziri ametoka Pemba hadi Kusini Unguja. Taasisi ya Afya Aga Khan na Wananchi kwa kujitokeza katika Maadhimisho ya Siku ya Saratani na Uongozi wa MIF kwa kufanya maandalizi.

Post a Comment

0 Comments