WAZIRI MCHENGERWA ATAKA MASHIRIKIANO SOKO LA KARIAKOO NA MWANAKWEREKWE ZANZIBAR.

 







Na mwandishi wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam Mhe. Albert Chalamila na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Visiwani Zanzibar Mhe. Idrissa Kitwana, Kuja na mpango mkakati wa kuunganisha soko la Kariakoo na Soko la Mwanakwerekwe ili kuhakikisha kuwa Masoko hayo yanakuwa na tija kwa wananchi wa Pande zote mbili za Muungano.

Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Soko la Mwanakwerekwe lililopo Mkoani wa Mjini Magharibi Visiwani Zanzibar na kumpongeza Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa umahiri wake na uzalendo katika kuwaletea wananchi Maendeleo kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani.

"Taifa lina bahati ya kuwa na Viongozi mahiri, wazalendo na wenye kujali maslahi ya wananchi hasa wale wa chini. Rais Mwinyi anafanya mambo makubwa na ya ajabu kwa maslahi ya Kizazi hiki na kizazi kijacho." Ameongeza Mhe. Mchengerwa.

Katika hatua nyingine Mhe. Mchengerwa akiwa mbele ya mamia ya wananchi walioshuhudia uzinduzi huo, amelitaja soko hilo kama kiungo muhimu cha kuinua uchumi wa wananchi wa Zanzibar, na kusema haya yote yanatekelezwa ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020/25.











Post a Comment

0 Comments