NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imezindua duka jipya ndani ya Kituo cha Treni ya Mwendokasi (SGR) jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kuimarisha jitihada za kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo lao Novemba 7, 2024 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuunga mkono maendeleo ya Taifa na kuwa imara katika kufikia mahitaji ya wateja wao.
"Uzinduzi wa duka hili siku ya leo unakamilisha mafanikio yatokanayo na mradi wa treni ya umeme ya SGR na wasafiri wanatumia usafiri huu kwa kuwa sasa wanaweza kupata huduma zote sehemu moja iwe ni huduma za miamala ya simu, simu za mkononi au msaada kutoka huduma kwa wateja. Hivi sasa wasafiri hawatokuwa na haja ya kutoka nje ya kituo kutafuta huduma za simu huku wakiwa na hofu ya kuachwa na treni. Kila kitu watapata humu ndani,”amesema Kadogosa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Airtel Tanzania, Eliud Sanga, amezungumzia umuhimu wa eneo duka hilo lilipo ikiwa ni sehemu ya malengo ya Airtel ya kuwawezesha watanzania na kupanua wigo wa mawasiliano na huduma za kifedha.
“Kuweka duka letu kwenye kituo kikuu cha SGR kunaimarisha lengo letu la kuwawezesha watanzania na kuwasaidia waweze kufikia ndoto zao. Kupitia uwepo wetu mahali hapa, tunafungua milango ya fursa kwa wasafiri, wajasiriamali na wakazi watakaokuwa wakipita katika kituo hiki kila siku. Lengo letu ni kuhakikisha kila mteja, anapata huduma na bidhaa zetu bila kujali mahali anapoelekea,” amesema Sanga.
Naye Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Adrianna Lyamba, amesisitiza kuwa kufunguliwa kw duka hilo la Airtel SGR jijini Dar es Salaam imekuja muda mfupi baada ya ufunguzi wa duka la Airtel katika kituo cha SGR mkoani Morogoro, hatua inayothibitsha azma ya Airtel kutoa huduma na bidhaa bora kwa wateja kwa ukaribu zaidi.
@airtel_tanzania
0 Comments