CPA MAKALA;CCM KUTUMIA 4R ZA RAIS SAMIA KATIKA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAAA.

 


Na mwandishi wetu

KATIBU wa İtikadi Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)CPA Amoss Makalla amewaomba wanachama wa Chama hicho nchi nzima kufahamu kuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu utaongozwa na R4 za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na hasa kuheshimiana na kuvumiliana.

CPA Makala ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM huku akifafanua Chama hicho kinaahidi kufanya kampeni za kistaarabu na ameviomba vyama vingine vya siasa nchini kampeni zitakapoanza waende na R4 ,wajenge  hoja.

“Tutofautiane tu kwa itikadi lakini tuna  Tanzania moja, uchaguzi uiache Tanzania ikiwa moja ya amani na utulivu.CCM tunavyosema hivyo tunamaanisha kwa mambo yaliyofanywa na Dk.Samia Suluhu Hassan kila Mwana ccm akipewa nafasi ya kuongea ataongea mambo Mengi yaliyofanywa.

“Kwahiyo kwetu sisi matusi hayata kuwa sehemu yetu ,kwetu sisi kejeli hazitakuwa sehemu yetu ,Tuna mambo mengi ya kueleza yaliyofanywa katika vijiji ,vitongoji na katika mikaa.”






#KaziIendelee

Post a Comment

0 Comments