*SEKTA YA MADINI NDIO SEKTA MAMA YA UCHUMI WA TANZANIA – DKT. KIRUSWA*
*_Dondoo za Mahojiano ya Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa katika Kipindi cha Kiss Ripoti - Kiss FM, Novemba 15, 2024_*
*Kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji wa Sekta ya Madini Tanzania 2024*
• Dhima: "Kuongezea Thamani Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii."
• *Malengo ya Mkutano:*
• Kutangaza fursa zilizopo katika sekta ya madini.
• Kubadilishana uzoefu na kukuza uwekezaji.
• Kujadili teknolojia za kisasa za uchimbaji na usafishaji madini.
• Kuhakikisha madini yanachangia katika uchumi kwa kuongezewa thamani.
*Nafasi ya Tanzania Katika Sekta ya Madini*
• Tanzania inaendelea na mkakati wa kuwa kitovu cha madini barani Afrika.
• Nchi nyingine zinajifunza kutoka Tanzania kuhusu usimamizi bora wa sekta ya madini mfano mzuri ni majirani zetu Malawi.
• Utafiti wa kina wa madini umeimarishwa, nanSerikali imewekeza zaidi katika miundombinu ya sekta.
*Mnyororo wa Sekta ya Madini:*
• Kuanzia utafiti, uchimbaji, usafishaji, biashara, na utoaji wa huduma migodini.
*Madini Mkakati:*
• Tumejaaliwa kuwa na aina nyingi za madini muhimu yanayohitajika kwa ajili ya nishati safi kama vile nikeli, kobalti, kinywe, gesi ya Helium na mengine.
• Madini muhimu kwa nishati safi ni nyenzo za kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
• Madini haya yanachangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi huku yakilinda mazingira.
• Mwekezaji yeyote anayekuja kuwekeza nchini lazima atuonyeshe mpango wa kuyasafisha au kuyaongezea thamani hapa hapa nchini madini muhimu.
*Uwezeshaji:*
• Tozo zimepunguzwa kutoka zaidi ya 30% hadi 9.3%.
• Wachimbaji wa dhahabu wanaotumia refineries za ndani wamepewa msamaha maalum wa kodi.
• Benki Kuu ya Tanzania sasa inanunua dhahabu ili kuimarisha akiba ya fedha za kigeni.
*Mfumo wa Masoko:*
• Masoko 43 na vituo vya ununuzi wa madini 105 yameanzishwa ili kuhakikisha wachimbaji wanapata uhakika wa soko na bei elekezi.
• Mfumo huu pia unasaidia kudhibiti utoroshaji wa madini na kuimarisha mapato ya serikali.
*Programu ya Mining for Brighter Tomorrow (MBT) inalenga vijana na wanawake kwa kuwapatia:*
• Vifaa vya uchimbaji ili wafanye shughuli zao kwa tija zaidi.
• Kuwapatia Leseni za uchimbaji ili wafanye shughuli zao bila usumbufu.
• Elimu kuhusu teknolojia na upatikanaji wa mikopo nafuu kupitia Taasisi za fedha na mabenki kwa uratibu wa serikali.
• Serikali kupitia STAMICO imeagiza mitambo ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo, mitano ilishawasili na kukabidhiwa wachimbaji wadogo na mengine 10 itawasili hivi karibuni.
• Msaada wa vifaa maalum, kama magari kwa kina mama.
*Mafanikio na Malengo ya Sekta*
• Sekta ya madini inachangia 9% ya Pato la Taifa (GDP), huku lengo likiwa kufikia 10% mwaka 2025.
• Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika kurasimisha sekta ya uchimbaji mdogo, jambo linalosaidia kukuza ajira na uchumi wa jamii.
*Ushirikiano wa Sekta ya Madini na Jamii*
• *Uchimbaji Mkubwa:*
• Kampuni kubwa zinatekeleza wajibu wa kijamii (CSR) kwa jamii zinazozunguka miradi yao kama vile ujenzi wa miradi kwa ajili ya huduma za kijamii, barabara, maji na kadhalika.
• *Utekelezaji wa Ushiriki wa Watanzania:*
• Mkazo umewekwa katika local content, kuhakikisha Watanzania wanashiriki moja kwa moja katika sekta ya madini kupitia ajira, huduma, na biashara.
• Hii ni sehemu ya jitihada za serikali kuifanya sekta ya madini kuwa kichocheo kikuu cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watanzania wote.
0 Comments