VIJANA WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUPINGA UKATILI, WAHIMIZWA KUSHIRIKI VYEMA CHAGUZI ZIJAZO.

 


Na. Abel Paul, Jeshi la Polisi Arusha.

Ikiwa ni mwendelezo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto elimu imeendelea kutolewa katika maeneo na taasisi tofauti tofauti Mkoani humo huku washiriki wa mafuzo hayo yaliyohusisha mbio fupi kutoka Taasisi ya uhasibu Arusha (IAA) wamehimizwa kushiriki pia katika uchaguzi wa serikali za mitaa na chaguzi zijazo.

Akiongea mara baada ya mbio hizo Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD) Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Georgina Matagi  amebainisha kuwa mafunzo na utoaji elimu juu ya vitendo ya ukatili vimeendelea kutolewa kwa makundi mbalimbali ili kukomesha vitendo hivyo.

SSP Georgina ameongeza kuwa alipata mwaliko wa jumuiya hiyo ya wanafunzi wa Taasisi ya uhasibu Arusha lengo likiwa ni kushiriki katika kampeni yao ya kuwahimiza vijana ushiriki wao katika uchaguzi wa mwaka huu na chaguzi zijazo.

Kwa upande wake Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Taasisi ya uhasibu Arusha Edwin Abiel amesema kuwa wamefanya mazoezi hayo ya pamoja lengo likiwa ni kuwakumbusha vijana wenzao kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa huku akiweka wazi pia kuwa mbio hizi ni kuwaleta karibu wanafunzi na Jeshi la Polisi ili kushirikiana katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili katika jamii.









Post a Comment

0 Comments