WANASIASA ZINGATIENI KANUNI NA MIONGOZO YA UCHAGUZI’ MHE. MCHENGERWA

 



Na mwandishi wetu


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka wanasiasa kuzingatia Kanuni, Miongozo  na Taratibu katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 27.

Muda wa kukata rufaa bado upo watu wasikae nyumbani na kuviacha vyama vyao kuendelea kuwasemea, rufaa inakatwa na mgombea mwenyewe kwahiyo wale wanaoona hawajatendewa haki watumie muda uliobaki wakakate rufaa,”amesema

Mhe. Mchengerwa amesema mgombea ambaye hajaridhika na mchakato njia ya kwanza ya kutafuta haki ni kuweka pingamizi kama hujapata haki yako kata rufaa kupitia kwa wasimamizi wasaidizi na hadi sasa bado wanasiku mbili kuwasilisha rufaa.

“Tujiepushe na mitandao ofisi ziko wazi hadi hivi sasa nazungumza 8:19 mchana ni waambie walioenguliwa wapeleke rufaa zao muda bado, kwakuwa mchakato bado kanuni zinanibana kuzungumza,”alisema 

Amesema uchaguzi wa Serikali za mitaa ni kalenda ya mwaka mzima kila siku kuna tukio lake na kanuni zinazotumika vyama vyote 19 vinavyotarajia kushiriki uchaguzi huo vilikaa pamoja na kukubaliana.

" waambieni wanasiasa wafuate utaratibu hatuwezi kuwa na taifa ambalo halifuati misingi ya Katiba,sheria, kanuni na taratibu tulizojiwekea wenyewe tutakuwa taifa la ovyo kabisa,”amesema 

Amesema hoja nyingi zinazoelezwa na vyama hivyo ni propaganda na inaonekana hawakujipanga na uchaguzi huo huku akieleza Novemba 14 mwaka huu atatoa tathimini na kutoa takwimu za kila mkoa kwa ushahidi.

Akijibu kuhusu ofisi kufungwa na wasiamamizi wasaidizi, Mheshimiwa Mchengerwa amesema taarifa zilizorekodiwa  kwa baadhi ya vyama vya upinzani ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),amejirisha pasipo shaka hazikufungwa.

“Ingawa kuna changamoto ilijitokeza katika mkoa wa Arusha kuna watu wasiokuwa na nia njema walivamia maeneo hayo na kutoa vitisho kwa watendaji, lakini maeneo mengi vituo vilikuwa wazi,”amesema 

Amesema kinachomshangaza ni kuona vyama vya siasa vinalalamika wagombea wao kuenguliwa wakati wagombea wenyewe wamebaki nyumbani hawapeleki rufaa zao.

"malalamiko wanayotoa kupitia viongozi wao kama wanacholalamikia ni kweli kanuni zetu ziko wazi ni nani anapaswa kwenda kukata rufaa, nawakumbusha kukata rufaa,” amesema  

Amesema kwenye vituo hakuna changamoto ila kinachofanyika ni propaganda za kisiasa kwa siasa kuhamia kwenye mitandao huku akieleza kumekuwa na viongozi wanaoaminika wanatumika kusambaza uvumi,”amesema 

Kwa upande wake, mwanasheria wa Tamisemi,Mihayo Kadete amefafanua maana ya ujasiriamali akisema ni kazi yeyote inayotambulika kiserikali huku akieleza si kigezo sawa cha kutumia kuwaengua wagombea.

“Si sahihi kwa mgombea wa chama chochote kuenguliwa kwa kigezo kama amejaza tu ujasiriamali ni kazi halali na yule aliyeenguliwa kwa kigezo hicho anapaswa kukata rufaa kutafuta haki yake,”amesema

Katika hatua nyingine,Meneja wa Kitengo cha Huduma za Utangazaji, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Andrew Kisaka amevihimiza vyombo vya habari kuzingatia usawa wa kurusha maudhui bila kuegemea upande wowote.






Post a Comment

0 Comments