📍 *Dar es salaam*
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameipongeza Wizara ya Madini kwa juhudi mbalimbali inazofanya za kuiendeleza Sekta ya Madini kufikia asilimia 9.0 katika kuchangia kwenye Pato la Taifa huku sekta ikikua kwa asilimia 11.3.
Ameyasema hayo, leo Novemba 19, 2023 wakati wa akifungua Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2024 unaendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa, uwepo wa Sera nzuri zenye ushawishi , mazingira salama yenye utulivu na amani, uwepo wa masoko ya uhakika yaliyounganishwa na jiografia nzuri vyote hivyo kwa pamoja vimekuwa vichocheo vikubwa katika ukuaji wa Sekta ya Madini nchini.
Waziri Mkuu Majaliwa amefafanua kuwa , Serikali itaendelea kuboresha miundombinu yote inayohusiana na mnyororo mzima wa thamani madini ikiwa barabara , nishati ya umeme pamoja kuongeza idadi ya vituo vya mauzo na masoko ili kuiweka sekta katika hali ya ubora na ushindani.
Awali, akimkaribisha Waziri Mkuu , Waziri wa Madini , Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa ili kuhakikisha Tanzania inaendelea kunufaika na rasilimali madini, Wizara imeendelea kuimarisha usimamizi wa shughuli za madini na kuhakikisha wananchi wananufaika naSerikali inapata mapato stahiki.
Akielezea kuhusu mwenendo wa ukusanyaji mapato Waziri Mavunde ameeleza kuwa, kiwango cha ukusanyaji maduhuli ya Serikali kimepanda kutoka Shilingi bilioni 624.61 kwa mwaka 2021 hadi kufikia Shilingi bilioni 753.83 kwa mwaka 2023.
Kuhusu ukuaji wa Sekta ya Madini , Waziri Mavunde amefafanua kuwa, kwa mwaka 2021 ukuaji ulifikia asilimia 9.3 ambapo mwaka 2023 sekta ilikuwa kwa asilimia 11.3 na mchango wake katika Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 7.2 hadi 9.3.
Naye , Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt. Mathayo David ameipongeza Serikali kwa juhudi mbalimbali inazofanya hasa katika kuendeleza Sekta ya Madini nchini kwa ushirikiano na sekta binafsi, hatua ambayo inaleta maana halisi ya kaulimbiu ya Madini ni Maisha na Utajiri.
Meneja Mkazi Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Barrick Dkt. Melkiory Ngido, amesema kuwa Kampuni Barrick inatambua mchango wa Serikali katika kuleta maendeleo na kwamba ipo bega kwa bega katika kuchangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa ambapo hivisasa Kampuni hiyo inajenga Barabara yenye Urefu wa Kilomita 73 kiwango cha lami , pamoja na kiasi cha shilingi Bilioni 70 katika ujenzi wa madarasa 1200 na mabweni 273.
Kwa upande wake, Makamu Rais wa AngloGold Ashanti anayeshughulikia Mahusiano na Maendeleo Endelevu (Afrika), Simon Shayo amesema , Kampuni ya GGM imeanza majadiliano na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuiuzia dhahabu pamoja na Mpango wa kutumia viwanda vya ndani vya kusafisha dhahabu.
*#MadininiMaishaNaUtajiri*
*#TMIC2024*
0 Comments