WAZIRI MKUU, MASAUNI WAFIKA SOKO LA KARIAKOO KUJIONEA SHUGHULI ZA UOKOAJI

 





 Na Mwandishi wetu- MoHA, Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameungana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kutembelea soko la Kariakoo, Dar es Salaam kujionea zoezi la uokoaji kwenye ajali ya ghorofa lililoporomoka leo Novemba 16, 2024.

Waziri Mkuu amesema hakuna mtu atakae achwa katika kifusi, hivyo amewataka watanzania kuendelea kuwa watulivu wakati zoezi la uokoaji likiwa linaendelea.

Post a Comment

0 Comments