KAWAIDA AZINDUA UVCCM KIJANI AWARDS

 



Na mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndugu Mohammed Ali Kawaida amewaongoza vijana katika uzinduzi wa tuzo (UVCCM KIJANA AWARDS) ambazo zitashirikisha Vijana waliofanya vizuri kwenye Sekta mbalimbali kwa mwaka huu. 

Uzinduzi wa tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na UVCCM zimeenda sambamba na uzinduzi wa UVCCM Alumni Forum umefanyika leo tarehe 21, Desemba 2024 eneo la Mbagala Zakhem, Dar es Salaam na utafuatiwa na matukio mbalimbali ikiwemo matukio ya kijamii na mchakato wa kuwapata watakaowania tuzo hizo ambazo hafla ya ugawaji wake itafanyika mwanzo mwa mwezi Feberuari 2025, na kwa upande wa UVCCM Alumn Forum Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu wa CCM, Emmanuel Nchimbi.

Akizindua tuzo hizo, Mwenyekiti wa  UVCCM, Mohamed Kawaida amesema;

“Tuzo hizi zisiwe tu za kuwatambua wale wanaoshinda lakini pia zitukumbushe kutafakari kwetu sote, je, tunawezaje kuhudumia Jamii zetu vizuri zaidi?, je, tunawezaje kuendelea kuchangia mafanikio ya Nchi yetu?, je, sisi Vijana wa Kitanzania tunawezaje kuchukua nafasi zetu za uongozi ndani ya UVCCM na Taifa kwa ujumla?, tukipata majibu ya hayo tunaweza kufikia malengo”

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UVCCM, Jokate Mwegelo amesema;

“Tuzo hizi hazilengi tu kuwaenzi waliofanya vizuri bali ni nyenzo ya kuhamasisha, kutia moyo, na kuhimiza kila kijana nchini Tanzania kuendelea kujitahidi kufanya vizuri kwa sehemu alipo, tuzo hizo zitatolewa kila mwaka na kila mwaka, tutatambua Wanachama katika vipengele mbalimbali vinavyoakisi kazi na michango yetu mbalimbali, iwe ni huduma bora kwa jamii, uongozi wa kibunifu, ujasiriamali wa Vijana, uanaharakati wa kijamii, au mafanikio ya kitaaluma”

Hii ni mara ya kwanza na ni historia inayoandikwa ndani ya UVCCM kuandaa tuzo na jukwaa hilo matukio ambayo yanaoenga kuibua ari kwa Vijana ndani na nje ya Jumuiya.











#KijananaKijani
#TunazimaZoteTunawashaKijani

Post a Comment

0 Comments