*RAIS MWINYI:SEKTA YA UJENZI IMETEKELEZA MIRADI MINGI NCHINI*
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amefahamisha kuwa Sekta ya Ujenzi ni miongoni mwa Sekta iliofanya vizuri katika Utekelezaji wa Majukumu yake kwa Kazi nzuri ya Ujenzi wa Madaraja, Barabara katika maeneo mbalimbali ya Nchi.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la Msingi la Barabara ya Kizimbani -Kiboje Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja yenye Urefu wa Kilomita 7.225 iliojengwa kwa Kiwango cha lami.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amefahamisha kuwa ni vema kwa Wananchi kutojenga katika eneo la Hifadhi ya Barabara ili libaki kwa Shughuli nyengine za kijamii ikiwemo kupitisha Miundombinu mengine ikiwemo Maji, Umeme na Mawasiliano .
Vilevile Rais Dk.Mwinyi amewasisitiza Wananchi wanaoishi Pembezoni mwa Barabara ya Kizimbani - Kiboje kufuata Sheria na kutojenga katika Eneo la Hifadhi ya Barabara hiyo.
Rais Dk.Mwinyi amesifu Kazi Nzuri iliofanywa na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mshauri Elekezi na Kampuni ya CCECC kwa kusimamia Ujenzi huo aliouelezea kuwa na Ubora na Viwango stahiki vya Barabara za Kisasa.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewanasihi Wananchi Kuendelea kuishi Kwa Amani na Umoja ili Nchi iendelee kutekeleza Miradi ya Maendeleo zaidi.
0 Comments