RAIS MWINYI:TUJIFUNZE ELIMU YA DINI

 



Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kwa Waumini kuweka mkazo katika kusoma na kutoa Elimu ya dini kwa dhamira ya  kunusuru jamii na  Changamoto za Kijamii.

Alhaj Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu  katika Sala ya Ijumaa na Kuufungua  Msikiti Mpya wa Chanjaani Mwanamashungi ,Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.

Alhaj Dk, Mwinyi amefahamisha  kuwa ni vema Misikiti ikatumika kwa Kusali , Kusoma Pamoja na kuitunza ili iwe na Mazingira mazuri  kwa Ibada.

Aidha , amewanasihi Waumini wa Dini ya Kislamu Kuitumia Misikiti Vizuri  Kukabiliana na  Changamoto Katika jamii.

Kwa upande mwingine Alhaj  Dk. Mwinyi  amewahimiza Waumini wa dini ya Kislamu,Viongozi wa Dini na Wanasiasa pamoja na Waandishi wa habari Kuhubiri Amani zaidì wakati nchi ikielekea katika Uchaguzi Mkuu.









Post a Comment

0 Comments