WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA AFRIKA KUHUSU KILIMO

 


Na mwandishi wetu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 11, 2025 ameshiriki Mkutano Maalum wa  Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika ambapo alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala Uganda.

Awali Mheshimiwa Majaliwa alishuhudia   Tamasha la Kahawa Afrika (Africa Coffee Festival) lililolenga kuhamasisha  uongezaji  thamani katika mazao yanayolimwa Afrika likiwemo zao la kahawa.





Post a Comment

0 Comments