#PICHA: Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohammed Ali Kawaida (@comrade_kawaida) ametembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Skimu ya maji Matamba - Kinyima katika kijiji cha Mbela wilayani Makete mkoani Njombe.
Kawaida ambaye yupo katika ziara mkoani Njombe amepokea taarifa ya mradi huo kutoka kwa Meneja RUWASA wilaya ya Makete Innocent Lyamuya ambaye ameeleza kuwa ujenzi wa tenki ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuchukua lita 50,000 na utasaidia kufikisha maji kwenye makazi ya watu wanaoishi maeneo ya miinuko.
Mradi huo ni unathamani ya shilingi Milioni 206 na unatarajiwa kukamilika Novemba 12, 2025 na Wananchi 1,015 wataondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji usioridhisha.
Kwa upande wa Mbunge wa Makete amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali Wananchi wa Makete kwani Wilaya hiyo inaongoza nchini kwa kupeleka maji vijijini.
0 Comments