DC KUBECHA AFIKA SOKO LA NGAMIANI , AELEKEZA MKANDARASI KUANZA KAZI KESHO IJUMAA

 


Na mwandishi wetu

Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe Japhari Kubecha Amefanya ziara katika Soko la Ngamiani Ikiwa ni Kwenda Kuona Adha Wanayopata Wafanyabishara Hususani Kipindi Hiki Ambacho Mvua Inakuwa Inanyesha.

Mara Baada ya Kufika Alitembelea Soko nzima pamoja na Wataalamu na Mkandarasi Kujionea Changamoto Mbalimbali Zilizomo Sokoni Humo lakini Kuwasikiliza Wafanyabiashara Nini Kifanyike kwa Haraka.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Baada ya Kusikiliza Alipata Wasaa wa Kutoa Maelekezo Mahususi kuhusu Soko Hilo , Alimuagiza Mkandarasi Kuanzia Kesho Ijumaa Ujenzi Wa Soko Uanze Haraka Iwezekanavyo Pia Akawaomba Wafanyabishara Kuwa na Subra Kupisha Ujenzi kwa Muda Mfupi Ili Uweze Kukamilika na Kuweza kufanya Shughuli zao Sehemu pazuri , Mwisho Kuwasihi Kuendelea Kuwa Watulivu kwani Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan Ipo Macho Wakati Wote na Muda Wote Kutatua Changamoto za Wananchi .


# *TANGA YETU ,LANGO LA UCHUMI WA AFRIKA MASHARIKI.*

Post a Comment

0 Comments