Na mwandishi wetu
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe Japhari Kubecha Amezindua Kampeni ya Upandaji Miti ya Matunda na Kivuli Zaidi ya Miche laki Moja [100,000] Kupandwa Kushirikiana na TFS pamoja na Wadau GIRL LED ACTION ON CLIMATE CHANGE.
Shughuli Hizo Zimefanyika Shule ya Sekondari Masechu Na Kuratibiwa na TFS ambao Wametoa Miche Laki Moja Lengo ni Kuhakikisha Tanga Inakuwa ya Kijani , Girl led Action on Climate Inaratibu Kuhakikisha Kampeni Hii Inafika Kwenye Mashule na Taasisi Mbalimbali Katika Kuendelea Kuhakikisha Tanga inakuwa ya Kijani.
Mheshimiwa Mkuu wa wilaya alipata Nafasi ya Kuzungumza na Wadau Kabla ya Zoezi la Upandaji wa Miti Kwa kuanza Kuwaomba TFS kuhakikisha Miche Watakayogawa kuzingatia Miche ya Matunda pia Kutoa Msisitizo kwa Wananchi wa Wilaya ya Tanga Kuhakikisha Tanga Inakuwa ya Kijani kwa Kila Mwananchi na Taasisi mbalimbali kupanda Miti ya Kivuli na Matunda Aidha Kuwasisitiza Wanafunzi nao Kila mtu Kuwa na Mche wake Na Kuhudumia Ili Kustawisha Wilaya ya Tanga Kuendelea Kushika hatamu kwenye Eneo la Usafi na Mazingira.
# *TANGA YETU ,LANGO LA UCHUMI WA AFRIKA MASHARIKI.*
0 Comments