JUSTIN J. MANIULA AJITOSA RASMI UBUNGE KAWE

 



*Dar es Salaam, Juni 28, 2025*


Ndugu Justin J. Maniula leo amefanikiwa kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika ofisi za chama hicho Wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Maniula amesema ameingia kwenye kinyang’anyiro hicho kwa dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Kawe na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

“Kawe ina changamoto lakini pia ina fursa nyingi za maendeleo. Niko tayari kusikiliza wananchi, kujifunza kutoka kwao na kuwasilisha maono ya mabadiliko chanya katika kila kata,” amesema.

Amesema kuwa anaunga mkono juhudi za maendeleo zinazoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kuwa yuko tayari kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo kwa manufaa ya wananchi wa Kawe.

Maniula amewahimiza wakazi wa Kawe kushirikiana naye katika safari hiyo akisema, *“Kawe ni yetu, maendeleo ni haki yetu na kupitia CCM, tunaweza.”*

Post a Comment

0 Comments