EWURA YATOA TAARIFA YA BEI BIDHAA ZA MAFUTA KUANZIA LEO JUMATANO APRILI 02,2025

 


TAARIFA KWA UMMA: Bei za bidhaa za mafuta ya petroli kuanzia Jumatano, tarehe 2 Aprili 2025, saa 6:1 usiku.


Kwa mwezi huu, gharama za uagizaji mafuta (premiums) zimepungua kwa wastani wa asilimia 6.08 kwa mafuta ya petroli, asilimia 7.09 kwa mafuta dizeli na kuongezeka kwa asilimia 1.11 kwa mafuta ya taa katika Bandari ya Dar es Salaam. 

Kwa Bandari ya Tanga hakuna mabadiliko, na kwa bandari ya Mtwara gharama zimepungua kwa wastani wa asilimia 4.00 kwa mafuta ya petroli na dizeli.

Aidha, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni (Applicable Exchange Rate) umeongezeka kwa asilimia 1.91.

#bei #petroli #beizamafutaAprili25 #jumatano #jumatanoyakwanzayamwezi #udhibiti #nishati #taarifa #taarifakwaumma








Post a Comment

0 Comments