MSAMA AWAOMBA WADAU KUJA KULISAPOTI TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU 2025

 


Na mwandishi wetu

Wadau mbalimbali na Watanzania wameobwa kujitokeza kwa wingi  kudhamini Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu litakalofanyika  katika mikoa 26 nchini

Akizungumza na waandishi wa Habari April 2, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion , Alex Msama amesema tamasha hilo halitakuwa na kingilo ili kila mtanzania aweze kushiriki kwenye kuliombea taifa huku maandilizi yakiwa yanaendele vizuri

 Msama ameongeza kuwa  tamasha litaanzia katika mkoa wa Dar es salaam na kwenda mikoa mingne na  limehusisha  Wachungaji, Maskofu wa mikoa mbalimbali katika kuhakikisha wanaombea amani kulekea uchaguzi Mkuu.

Aidha amesema waimbaji mbalimbali wakubwa kutoka nje ya nchi na Ndani ya nchi watakuwepo kwenye tamasha la Kuombea Uchaguzi.

" Tutatangaza tarehe na eneo  ambalo tamasha hili litafanyika hivi karibuni  kwa mkoa wa Dar es salaam  ambapo tamasha hili ndipo litakapo anzia" amesena Masama

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Barazaa  Makanisa ya Kipenteksote Mkoa  wa Dar es salaam, Mch  Emmanuel Mwasota amesema  tamasha hilo lipo kwajili ya Maombi ya Kuombea uchaguzi Mkuu kwa kuungana kwa pamoja kwa waumi wote wa madhehebu yote kuiombea nchi yetu, viongozi , wabunge, madiwa na Rais wetu ili chaguzi uweze kupita kwa amani

"Sisi tumesema ya kwamba tutashikama kwa pamoja na taarifa hizi zinaenda kila mahali kwa  makanisa, wachungaji, maskofu na waubiri wa aina mbalimbali tutakuwa kwa Pamoja kwaajili ya  kuhakikisha tunaombes nchi yetu ipite salama kwenye uchaguzi utakaofanyika mwaka huu"

Ameongeza kuwa uchaguzi unaweza kusabisha nchi inaweza ikapasuka kama raia  wake wasipokuwa wazalendo hasa kwa upande wa amani kwajili ya kuombea nchi na viongozi wetu ambao wanatuongoza katika maswala ya nchi yetu na sisi tunahitaji amani na maombi ili tuweze kuvuka kwenye uchaguzi kwa  amani

Post a Comment

0 Comments