RC MALIMA AWAKARIBISHA MAAFISA MAWASILIANO MKOANI MOROGORO.

 



Na Mwandishi wetu, Morogoro.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amewakaribisha maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa serikali wanaotarajia kukutana kwenye mkutano wao  wa mwaka utakofanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 8-12 aprili, 2025.

Mhe. Malima ameyasema hao leo tarehe 3 aprili, 2025 wakati wa kikao cha pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali katika ofisi yake.

Amesema kama mkoa ameupokea mkutano huo na itakuwa faraja kwa wananchi wa Morogoro kwani ni jambo kubwa kufanyikia mkoani kwake, “Mimi ni mdau mkubwa wa mawasiliano tangu zamani, hivyo mkutano huo ni muhimu kwani afisa mawasiliano ni nafasi kubwa kwenye ngazi serikalini ambapo mtajengewa uwezo na hivyo kunyoosha na kutoa habari kwa wananchi kwa usahihi”.

Hata hivyo Mhe. Malima amewataka maafisa mawasiliano wanaoshiriki mkutano huo kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo kwenye Mkoa huo ukiwemo hifadhi ya Taifa Mikumi pamoja na hifadhi ya milima ya Udzungwa.

Mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha maofisa mawasiliano wa serikali unatarajiwa kufanyika Morogoro katika ukumbi wa hoteli ya Morena kuanzia tarehe 8 hadi 12 aprili, 2025.



Post a Comment

0 Comments