SHAMIRA ACHANGIA UJENZI NYUMBA YA KATIBU UVCCM GAIRO- MOROGORO.

 


Na mwandishi wetu

 Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa Viti Vitatu Tanzania Bara Ndg. Shamira Mshangama @shamiramshangama akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ameshiriki kama mgeni rasmi kufungua kikao cha Baraza la UVCCM Wilaya ya Gairo na  kufanya zoezi la ukaguzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro.

Akiwa katika ufunguzi kikao cha Baraza Shamira amesisitiza vijana kujipanga kuelekea kuzitafuta kura za CCM na kukipatia chama ushindi. 

Katika ziara hio ya Mkoani Morogoro amewakabidhi Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) pesa kwa kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Morogoro Wilaya ya Gairo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Rajab Magota kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya katibu wa UVCCM Wilaya ya Gairo. 

Amewaeleza vijana kuwa pamoja na kazi zote tunazofanya lakini viongozi tunajukumu la kuzingatia ujenzi wa CCM na Jumuiya zake.

Post a Comment

0 Comments