TUME YA MADINI KUENDELEA KUWASAIDIA WASAMBAZAJI NA WAUZAJI BARUTI.

 



Na mwandishi wetu

Tume ya Madini imesema itaendelea kutoa ushirikiano na kuwasaidia wasambazaji na wauzaji wa baruti nchini ili wafanye shughuli zao kwa mujibu wa Sheria na kanuni za baruti zilizopo.

Mkaguzi Mkuu wa Migodi Mhandisi Hamisi Kamando amesema hayo leo Aprili 4, 2025,Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi kilichowakutanisha  wadau wa baruti, pamoja na Wakaguzi wa Migodi na Baruti Nchini.

Mhandisi Kamando amesema kutokana na ongezeko la shughuli za uchimbaji wa madini kumepelekea kupanuka kwa biashara ya baruti hapa nchini.

“Ongezeko la uhitaji wa matumizi ya baruti hapa nchini imepelekea uwepo wa changamoto kadhaa katika usimamizi wake,hivyo watumishi wa Idara ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira kutoka Tume ya madini wataendelea na udhibiti katika maeneo yao ili kuepusha madhara,amesema.

Ametoa wito kwa wadau wa baruti nchini kujiunga katika Chama Cha Wauza Baruti Tanzania (TEDA), ili  Serikali iweze  kuwasaidia kwa pamoja.

Mdau wa Baruti kutoka Mkoa wa  Geita Mhandisi  Ramadhani Kamaka ameeleza kunufaishwa na kikao hicho na kuiomba Serikali kutoa elimu zaidi kwa mamlaka ambazo zinahusika  katika usimamizi wa baruti nchini.





Post a Comment

0 Comments