DC Mwanziva akemea uuzaji wa gesi pungufu

 


Na mwandishi wetu

Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mh. Victoria Mwanziva, (aliyesimama, pichani) amekemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wa gesi ya LPG ya kuuza gesi yenye uzito pungufu, akisema tabia hiyo inadhulumu haki za wateja wao.   

Mh. Mwanziva ameyasema hayo leo tarehe 6/5/2025, alipokuwa akifungua semina ya EWURA kwa mawakala wa gesi ya LPG mkoani Lindi. 

Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Mhandisi Nyirabu Musira, amesema semina hiyo ni sehemu tu ya jitihada za EWURA kuhakikisha wafanyabiashara wanaendesha shughuli zao katika namna inayojali usalama, afya na mazingira.



Post a Comment

0 Comments