UTAMBULISHO WA MGOMBEA URAIS WA CHAMA CHA HAKI NA MAENDELEO (CHAUMMA)


 

Dar es Salaam, 21 Mei 2025

Chama cha Haki na Maendeleo (CHAUMMA) kinapenda kuwataarifu wanachama wake, wapenzi wa chama, na umma kwa ujumla kuwa, katika kikao chake cha Kamati Kuu kilichofanyika tarehe 10 Mei 2025 jijini Dar es Salaam, uamuzi ulifikiwa kwa kauli moja kumteua Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chetu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Uteuzi huu ulithibitishwa na kuidhinishwa rasmi na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa uliofanyika siku hiyo hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo wajumbe wote walionesha imani kubwa kwa Mheshimiwa  Freeman Aikaeli Mbowe kupeperusha bendera ya CHAUMMA katika nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi.

Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe ni mwanasiasa mwenye uzoefu mkubwa, uadilifu, na maono ya kuleta mabadiliko chanya kwa taifa letu. Uteuzi wake unaashiria dhamira ya CHAUMMA ya kuleta uongozi bora, unaojali maslahi ya wananchi, na wenye kujenga misingi imara ya haki, usawa, na maendeleo endelevu.

Chama kinatoa wito kwa wanachama wote, wapenzi wa chama, na wananchi kwa ujumla kuungana nasi katika kumuunga mkono Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe katika safari hii ya kuelekea Ikulu, kwa lengo la kuleta mabadiliko tunayoyatamani.

Tunaamini kuwa kwa pamoja, tutaweza kujenga Tanzania mpya yenye matumaini, haki, na maendeleo kwa wote.

Post a Comment

0 Comments