DC KUBECHA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA WILAYA YA HANDENI ASISITIZA USHIRIKIANO , UMOJA NA KUHAMASISHA WANACHI KUJITOKEZA KWENYE MWENGE WA UHURU

 


Na mwandishi wetu

Mkuu wa wilaya ya Handeni Mhe Japhari Kubecha Leo Amekutana na Watumishi wa Halmashauri zote Mbili kwa Malengo Mawili Tofauti Mojawapo ni Kujitambulisha kwao lakini Kuzungumzia Maandalizi ya Mwenge Kiwilaya Ambapo Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Handeni Utakuwa Tarehe 6 na 8 Mwezi wa 6 .

Aidha Ziara Hiyo  ilianza katika Halmashauri ya Handeni Mji na Kukutana na Kamati ya Mwenge kuzungumzia maandalizi ya Mwenge na Kujitambulisha kwa Watumishi wa Halmashauri hiyo , Baada ya Hapo kwenda Halmashauri ya Handeni Vijijini na Kukutana na Kamati ya mwenge pamoja na Watumishi na Kusema nao.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Alianza kwa Kuwashukuru kwa Mapokezi Mazuri lakini Aliwaomba Ushirikiano katika Kufanya kazi  , Pia akasisitiza Wananchi Kuhamasishwa Kujitokeza kwa Wingi Kushiriki Mwenge wa Uhuru na  Kuwakumbusha  Kuendelea Kuwasikiliza na Kuwahudumia Wanachi Wa wilaya ya Handeni wakati Wote kwa Bidii . 


 *# HANDENI YETU , MAENDELEO YETU*

Post a Comment

0 Comments