Na mwandishi wetu
Dar es Salaam, Juni 28, 2025 — Ndugu Geofrey Timoth leo amechukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge wa Jimbo la Kawe, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Timoth amesema dhamira yake kubwa ni kuboresha maendeleo ya Jimbo la Kawe, huku akieleza kuwa changamoto kubwa inayolikabili jimbo hilo kwa muda mrefu ni miundombinu mibovu ya barabara.
“Nimeamua kuingia katika kinyang’anyiro hiki ili kuwatumikia wananchi wa Kawe. Kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya barabara duni, jambo ambalo linaathiri shughuli za kiuchumi na kijamii. Nawaahidi wananchi kuwa nitahakikisha tatizo hili linapatiwa ufumbuzi wa kudumu,” alisema Timoth.
Mchakato wa uchukuaji fomu kwa nafasi ya ubunge umeendelea kuvutia wanademokrasia mbalimbali katika Wilaya ya Kinondoni, huku wagombea wakiahidi kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.
0 Comments