KAWAIDA AKAGUA MRADI WA VIJANA KASEKESE

 



Na mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) amekagua Mradi wa Godauni ya kukoboa na kutunza mpunga, wa Vijana wajasiriamali wanaofaidika na mkopo wa asilimia 10 kutoka Halmashauri wa Kiasi Cha Shilingi Milioni 61 katika eneo Kasekese, Wilaya ya Tanganyika leo Alhamisi 12 Juni, 2025.

Mwenyekiti Kawaida amewataka Vijana wanufaika wa mikopo ya Halmashauri kuwa wazalendo wa kurejesha mkopo Kwa wakati iliuweze kuwasaidia Vijana wengine wenye uhitaji. 

Aidha, kawaida ameongeza Kwa kusema Viongozi wa Maendeleo ya Jamii wasikae ofisini, bali waende katika maeneo yenye wanufaika ili kukagua Maendeleo ya Miradi Kwa Maendeleo endelevu.

Ni siku ya pili ya Kibabe ya ziara ya Mwenyekiti Kawaida katika Mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe ambapo ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM TAIFA.

Vijana Tunasema 

OKTOBA TUNATIKI ✅✅✅ 




#KaziNaUtuTunasongaMbele

#TunazimaZoteTunawashaKijani

#OktobaTunatiki✅✅✅

Post a Comment

0 Comments