RIDHIWANI KIKWETE AHUTUBIA MKUTANO WA VIJANA WA DUNIA- CHINA, AELEZA ULIMWENGU MIKAKATI YA TANZANIA KUWEZESHA VIJANA

 




_Agusia mikopo ya 10%, fedha 30% za manunuzi, kushusha riba kwa wakopaji na sera imara za Tanzania kuinua Vijana n.k_

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete Jana Julai 20, 2025 ameshiriki na kuhutubia Mkutano wa Vijana Wa Dunia uliofanyika katika Mji wa Suzhou, China.

Kwenye Mkutano huo mkubwa wa Dunia, Kikwete ameweka wazi hatua mbalimbali ambazo zimefikiwa na Serikali ya Awamu ya 6 ya  Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwawezesha vijana ikiwemo msisitizo mkubwa uliowekwa kisera, kisheria na mipango mbalimbali ya kimaendeleo na ushirikishwaji wa vijana ikiwemo ile ya mgawanyo wa asilimia 10 za mapato ya ndani ya Halmashauri na 4 kwa Vijana, asilimia 30 za fedha za manunuzi ya umma, mikopo ya uwezeshaji wa umma ikiwemo ya NEEC, BEST, na hatua ya kushusha riba kwa wakopaji katika mabenki ya biashara, uundaji wa Sera Mpya ya Vijana Nchini, Programu za maendeleo kama BBT- Madini, Kilimo, Mifugo ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa kwa sasa kwa Vijana wa Tanzania. 

Mkutano huo uliomalizika kwa mafanikio makubwa unakuwa ni mkutano wa 14 kukutanisha nchi wanachama na unafungua fursa kwa nchi wanachama kukutana na kupeana uzoefu katika kushughulikia changamoto mbalimbali zinazokabili vijana Duniani.




Post a Comment

0 Comments