Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi kimewataka wana CCM kutambua uchaguzi mkuu si jambo la dharura na ghafla hivyo kila MwanaCCM ajue wakati umefika wa kusimama pamoja kutafuta ushindi wa chama.
Pia chama hicho kimewahimiza wanachama wake wote , kujitokeza itakapoanza ngwe za kampeni na siku ya upigaji kura kwani uchaguzi ni suala la kufa na kupona.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis ametoa maelezo hayo huku akiwataka wanachama wote kushiriki kwa nguvu zote kuwachagua wagombea toka CCM.
Mbeto alisema ni muhimu kwa kila mwanachama wa CCM ajue kuwa kujitokeza kwao siku ya kupiga kura ,wajione wamebeba urithi wa wazazi unaotokana na vyama vya TANU na ASP vilivyoleta Uhuru na Mapinduzi.
Alisema Uchaguzi ndio unaoviweka Vyama vya Siasa madarakani hivyo anawahimiza wananchi wa Tanzania na Zanzibar , kwenda kuwapigia kura wagombea Urais wa CCM, Dk Samia Suluhu Hassan na Dk Hussein Ali Mwinyi .
"Uchaguzi si jambo na zoezi la ghafla. Kila baada ya miaka mitano hufanyika. Pamoja na CCM kuionyesha dunia nchi zetu zinaongozwa kidemokrasia . Matumaini yote ya wananchi yamebebwa na sera CCM si vinginevyo" Alisema Mbeto
Aidha, Katibu huyo Mwenezi alisema kipimo cha kuchaguliwa tena Marais Dk Samia na Dk Mwinyi kinatokana na ufanisi wa kazi kubwa walizozifanya miaka mitano iliopita.
'CCM kinashiriki Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2025/2030 kikiwa na matumaini makubwa ya kushinda kuliko miaka yote . Kitashinda baada ya kimtetimiiza wajibu na ahadi zake kwa jamii na kwa maendeleo ya nchi "Alisema Mbeto
Pia alisema kutokana na kufanyika kazi kubwa iliotokana na utendaji wenye ufanisi na utekelezaji wa kisera, CCM kitashiriki uchaguzi huo oktoba kwa lengo moja tu la kushinda na kuongoza dola.
"Tumetekeleza ahadi zetu zote kama chama tawala . Marais wetu wametoka jasho na kutimiza wajibu kwa vitendo na utumishi uliotukuka. Kazi iliobaki ipo kwa wananchi wanaosubiri kutia tiki katika karatasi za kura" Aliileza
Hata hivyo Katibu huyo Mwenezi alisema Chama Cha Mapimduzi lazima kishinde kwakuwa kinaaminiwa na Wananchi waliio wengi ,kina viongozi Wazalendo, sera makini na Siasa safi .
"Chama chetu hakisubiri kudandia au kuvizia wagombea wanaotemwa na vyama vingine ili wagomba urais na ubunge . Tuna mamia ya wagombea madhubuti wanaoeleweka na Wazalendo wasiotiliwa shaka yoyote "Alisiaitiza Mbeto
0 Comments