Dar es Salaam, Tanzania – 7 Septemba 2025
Mwenyekiti wa Chama cha Biashara na Viwanda cha Oman, Dkt. Salem Al-Junaibi (Mb), pamoja na ujumbe wake wa wafanyabiashara, amewasili nchini leo kwa ziara ya siku tano, ikiwa na lengo la kuchunguza fursa za uwekezaji na biashara katika sekta mbalimbali za Tanzania.
Mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dkt. Al-Junaibi na ujumbe wake walipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Twaibu, pamoja na Balozi Abdalah Kilima, Mkurugenziwa Idara ya Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Viongozi wengine waliokuwemo ni Naibu Balozi wa Oman nchini Tanzania, Rashid Al Mandhir, pamoja na maafisa waandamizi kutoka Serikali na Sekta binafsi.
Ziara hiyo itahusisha mikutano na taasisi mbalimbali za umma na binafsi, zikiwemo:
-
Tume ya Ushindani (FCC)
-
Kiwanda cha Nyama – Kibaha
-
Chamber of Commerce, Industry and Agriculture Tanzania (TCCIA)
-
KAMAKA, TISEZA, BRELA, TANTRADE, TBS, TIRDO, NDC
-
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)
Bodi ya Chai Tanzania (TTB)
Aidha, ujumbe huo utakutana na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Nishati, pamoja na Ofisi ya Rais – Kazi, Uchumi na Uwekezaji, na kusaini mikataba ya ushirikiano kati ya Tanzania na Oman.
Baada ya Dar es Salaam, ziara itahusisha ziara Zanzibar ambapo wajumbe watafanya mazungumzo na viongozi wa ZIPA, ZNCC, pamoja na kutembelea Eneo Maalum la Uchumi Zanzibar.
Pia, ujumbe wa Oman utatoa mawasilisho kuhusu hali ya biashara na viwanda nchini Oman na fursa za ushirikiano zaidi kati ya nchi hizo mbili.

Ziara ya Dkt. Al-Junaibi na ujumbe wake inatarajiwa kumalizika tarehe 12 Septemba 2025, kabla ya kurejea Oman.
0 Comments