Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mgombea wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 6 Septemba 2025 amerejesha rasmi fomu za uteuzi katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Katika hotuba yake fupi baada ya zoezi hilo, Dkt. Mwinyi aliwashukuru wanachama wa CCM kwa kumdhamini na kumuwezesha kufanikisha hatua ya kurejesha fomu. Aidha, aliwataka wagombea wote kuendesha kampeni za kistaarabu na kuhubiri amani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ZEC, Jaji George Joseph Kazi, alisema baada ya zoezi la urejeshaji wa fomu, hatua inayofuata ni uhakiki na kushughulikia pingamizi kabla ya kutangaza majina ya wagombea rasmi.
Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar zinatarajiwa kuanza tarehe 13 Septemba 2025, na uchaguzi wenyewe kufanyika Oktoba 29, 2025.
0 Comments